TAMSYA mkoa wa PWANI A umefanikiwa kuadhimisha Siku ya Hijab (HIJAB DAY) katika kilele cha mkoa ambapo ilifanyika katika wilaya ya Bagamoyo, ndani ya Ukumbi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa).
Mgeni Rasmi MH. CPA SUBIRA MGALU, MBUNGE WA JIMBO LA BAGAMOYO aliungana nasi katika kufanikisha maadhimisho ya haya kwa kuungana na TAMSYA mkoa wa PWANI A kuwavisha mabinti 60 waliokuwa na uhitaji wa Hijab ukumbini ambazo zilipatikana kwenye harambee iliyosimamiwa na viongozi wa TAMSYA mkoa wa PWANI A.
Pia mgeni rasmi aliahidi kuchangia hijab 40 ili kutimiza mabinti 100 watakaovishwa hijab kwenye maadhimisho haya. Sambamba na hilo mgeni rasmi aliipokea risala iliyowasilishwa na mwakilishi wa Amirat TAMSYA mkoa wa PWANI A, ambapo katika sehemu ya kujibu risala hii Mgeni rasmi aliahidi kuchangia Cherehani nyingine nne(4) pamoja na mashine moja(1) ya kudarizi ili kuwezesha mradi wa ushonaji uliopo Kisarawe na kuboresha mafunzo yanayotolewa katika mradi huu pia kuanzisha vituo vingine vya ushonaji katika kila wilaya.
TAMSYA mkoa wa PWANI A unatoa Shukrani kwa kuwaombea dua kila mmoja aliyeshiriki kufanikisha maadhimisho haya pamoja na wale walioungana na viongozi wa mkoa kuchangia upatikanaji wa hijab hizi Allah s.w awafungulie milango yao ya rizq na awafanikishe majambo yao (Amiyn).
Wabillah tawfiyq