Mon - Sun: 09 AM - 09 PM

ZIARA YA VIONGOZI WA TAMSYA MAKAO MAKUU KWENYE UBALOZI WA SAUDI ARABIA

Walioshiriki ziara hiyo ni Kassim Ibrahim - Rais, Buliba Magambo - Katibu Mkuu, Yusuph Abdul - Mjumbe Idara ya Elimu, Abdulhakim Abdallah - Afisa Habari mnamo Tarehe 12/10/2022 Jumatano.

AGENDA ZILIZOJADILIWA
1. Kuitambulisha TAMSYA na Kazi zake
2. Kuimarisha ushirikiano wa TAMSYA na Ubalozi wa Saudia Arabia
3.Fursa za Udhamini na scholarship mbalimbali zinazotolewa na vyuo vya Saudia Arabia
4.Miradi mbalimbali inayosimamiwa na TAMSYA na kuhitaji udhamini hususani mradi wa Buyuni.
5.Fursa ya vijana kwenda Kutekeleza Ibada ya Hija na Umrah

MAJADILIANO
Viongozi walianza na utambulisho ufupi wa TAMSYA pamoja na nafasi zao Mheshimiwa Balozi Abdullah Al Sharyan aliwasikiliza Kwa umakini viongozi wa Kazi za TAMSYA na maeneo mbalimbali ambayo TAMSYA ingependa kupata ushirikiano na Ubalozi sambamba na Kuimarisha mahusiano kati ya TAMSYA na Ubalozi wa Saudi Arabia

Kuomba fursa za scholarship kwa wanafunzi na vijana wa kiislam nchini Saudi Arabia. Muheshimiwa Balozi sambamba na wasaidizi walitupatia list ya vyuo 26 vinavyotoa udhamini wa masomo katika fani mbalimbali za Afya,uchumi,uhandisi,Tiba na masomo ya Dini Sambamba na hilo Muheshimiwa Balozi na wasaidizi wake walitupa vigezo vya kupata fursa hiyo kwa ngazi ya Shahada,Shahada ya uzamili na Shahada ya uzamivu

Nukta nundu Mh Balozi alifafanua Kwa lugha ya upole kwamba fursa zinakuja nyingi lakini wanaomba ni wachache Sana. Aidha baada ya mazungumzo Mheshimiwa Balozi alitaka tuwasilishe maombi mbalimbali kwa njia ya barua katika ofisi ya Ubalozi na kuahidi kujenga ushirikiano wa karibu na TAMSYA.
Pia vijana wamehimizwa kuchangamkia fursa za nafasi 100 za scholarship nchini Saudia Arabia ambazo zinagharamikia kila kitu ikiwemo hela ya kujikimu kila mwezi.

Viongozi walifanikiwa kumualika Muheshimiwa Balozi kwenye mkutano mkuu wa TAMSYA wa mwaka huu na Balozi alisema Yuko tayari kujumuika nasi.

Katika kuhitimisha mazungumzo Rais wa TAMSYA alimkabidhi Mh Balozi zawadi ndogo iliyoandaliwa Kwa ajili ya kumbukumbu na muambata wa Balozi alihimiza Sana kutuma maombi yetu kwa njia ya Maandishi.