Mon - Sun: 09 AM - 09 PM

UZINDUZI WA TAMSYA DODOMA CENTRE

Hatimaye Ile kiu kubwa ya viongozi wa TAMSYA Mkoa wa Dodoma ya kuhakikisha Wanafunzi na vijana wa Kiislamu Mkoa wa Dodoma wanakuwa na kituo Chao Maalumu Cha Elimu inakwenda kukamilishwa kwa Uzinduzi wa Majengo ya Msikiti, Vyumba vya Madarasa pamoja na Nyumba ya Mwalimu katika Eneo la TAMSYA lililopo Chidachi Dodoma.

Mwaka 2019 Mwl Jafar Daya Alikabidhiwa Uongozi wa kuongoza Jumuiya ya Wanafunzi na vijana wa Kiislamu TAMSYA Mkoa wa Dodoma, Baada ya kukabidhiwa majukumu hayo jambo la kwanza ilikuwa ni kuhakikisha Eneo la TAMSYA lenye Hekari takribani 7 lililopo Chidachi linaendelezwa kwa kujenga Kituo cha Elimu ambacho kitawakutanisha vijana na Wanafunzi wa Kiislamu Mkoa wa Dodoma na wale waliopo nje ya Mkoa huo.

Amir Mwl Jafar Daya aliamini ili kufikia malengo hayo ni kuunda Safu imara ya Uongozi ambao utakuwa na hari ya kufanya kazi Kwa vitendo, mchakato wa Kwanza ilikuwa ni kuhakikisha Deni la Tsh Milion 15 linalipwa kwaajili ya kupata Hati miliki.

Mwenyekiti wa TAMSYA Mwl Jafar Daya pamoja na Viongozi wengine waliamini kuwa Eneo lililopo Chidachi ni mali ya Wanafunzi na vijana wa Kiislamu hivyo Kila mmoja wao awajibike kwa nafasi yake ndipo likaja wazo la kuchangia Mchango wa Tsh 1,000 kwa kila Mwanafunzi wa Sekondari na Vyuo bila kusahau michango ya Wadau mbalimbali.

Maoni ya Watu yalikuwa mengi huku wengi wao wakiamini vijana wataishia njiani Wala hawataweza kufanikisha Jambo hilo.

Kwakuwa TAMSYA Ina Idara zake za kiutendaji ndipo Idara ya Habari uhusiano na ustawi wa jamii ikapewa jukumu la kuanza kuzunguka kwa Wanafunzi Kila Kona ya Mkoa wa Dodoma kuwaelewesha jambo hilo.