Uongozi wa shule ya Kisaza High School iliyopo kijiji Cha Kwamkonga wilayani Handeni mkoani Tanga, usema umefurahishwa na ziara iliyofanya na uongozi wa TAMSYA mkoa wa Tanga.
Akizungumza wakati semina fupi kuelekea maandalizi ya mitihani ya Taifa iliyoratibiwa na TAMSYA, makamu mkuu wa shule hiyo ameshukuru TAMSYA kufika na kutoa mchango wao wa kitaaluma ambao utasaidia wanafunzi kipindi hiki cha maandalizi.
Aidha Mwl, Jamal Hassan Mangare amabaye ni mkuu wa idara ya vijana amewataka wanafunzi kuweka mikakati ya muda mfupi ili kuhakikisha wanafaulu mitihani yao. Kwa upande wake Mwl, Amina Toba ameusia wanafunzi wa kike kuhakikisha wanazifuta machozi familia zao kwa kufanya vizuri katika masomo na tabia kwa kuwa kioo kizuri cha jamii. TAMSYA imefanya ziara shule sekondari Kisaza ikiwa ni muendelezo wa semina elekezi kwaajili maandalizi ya mitihani kwa vidato vinavyofanya mitihani ya Taifa.