TAMSYA mkoa wa PWANI ZONE A kwa siku mbili yaani JUMAMOSI TAREHE 04-10-2025 na Jumapili TAREHE 05-10-2025 wameendesha na kuzisimamia MAHAFALI za wahitimu wa KIISLAMU KIDATO CHA NNE katika maeneo matano tofauti yaani:
Mahafali ya pamoja shule za sekondari zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Kibaha iliyofanyika VIWANJA VYA SHULE YA SEKONDARI KILANGALANGA
Mahafali ya wahitimu wa kiislamu kidato cha nne kutoka shule za sekondari zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Chalinze iliyofanyika Ukumbi wa POLISI - Chalinze
Mahafali ya pamoja ya wahitimu kidato cha nne kutoka shule za sekondari zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo iliyofanyika viwanja vya shule ya sekondari Matimbwa
Mahafali ya wanafunzi wa kiislamu Shule ya Sekondari Magindu
Mahafali ya wahitimu wa kiislamu kutoka shule ya sekondari East Coast. Aidha mahafali haya yalifanikiwa kuwa mubashara kwenye baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo TV Imaan pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii.
Allah awalipe kher wale wote waliotuunga mkono kusimamia na kuendesha mahafali hizi kwa ufanisi ulio bora kabisa
Wabillah tawfiq