TAMSYA-ISLAMIC KNOWLEDGE PROGRAM.
Uongozi wa TAMSYA wilaya ya kilombero umeendelea na ziara Yake ya kutembelea matawi na kufatilia shughuli nzima ya ufundishaji wa Elimu ya dini ya kiislamu.
Aidha katika ziara hiyo Uongozi wa TAMSYA wilaya ya kilombero chini ya kaimu Naibu Amir wa TAMSYA wilaya ndugu RASHID KHAMIS amefanikiwa kutembelea baadhi ya shule za msingi zinazopatikana hapa Ifakara na kuweza kugawa vitabu vya maarifa ya uislamu E.D.K , katika shule ya msingi mapinduzi, Ifakara na muhola.
Aidha zoezi Hilo litaendelea kufanyika Kesho kwa shule mbalimbali za sekondari ndani ya wilaya ya kilombero.
Vilevile tunawaomba wadau mbalimbali kuweza kutuchangia vitabu kwa ajili ya kuweza kusapoti suala zima la ufundishaji wa islamic knowledge mashuleni.
Mwisho Uongozi wa TAMSYA wilaya ya kilombero utaendelea kutembelea matawi mbalimbali ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanafunzi na vijana wa kiislamu ili kuweza kupambana na ujinga, umaskini,maradhi pamoja na mmonyoko wa maadili.
Imetolewa na.
AYOUB JUMA MKONDO
AMIR TAMSYA WILAYA YA KILOMBERO