TAMSYA GRADUATION PROGRAM -KILOMBERO

Uongozi wa TAMSYA Wilaya ya Kilombero umefanikiwa kuandaa na kufanikisha mahafali ya pamoja ya wanafunzi wa Kidato cha Nne na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (FDC).

 

Mahafali hayo yalifanyika siku ya Jumapili, tarehe 05 Oktoba 2025, katika Ukumbi wa Maendeleo ya jamii, yakihusisha jumla ya wahitimu 160. Zaidi ya wanachama 500 wa TAMSYA kutoka maeneo mbalimbali walihudhuria na kusherehekea pamoja na wahitimu.

 

Aidha Mwenyekiti wa Idara ya Elimu TAMSYA Mkoa wa Morogoro, Ndugu KURWA MOHAMED, aliwasihi wanafunzi kuongeza juhudi katika kipindi hiki kifupi kilichosalia kabla ya mitihani yao ya mwisho, akisisitiza umuhimu wa nidhamu na bidii.

 

Pia Msaidizi wa Sheikh wa Wilaya ya Kilombero, SHEIKH KHALIFA, aliwatia moyo wanafunzi na vijana wa Kiislamu kuendelea kumtegemea Allah (S.W.), na pia kuendeleza kujifunza elimu ya Dini ya Kiislamu hata baada ya mitihani.

Aidha Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba , MADAM HAWA, aliahidi kushirikiana kwa karibu na uongozi wa TAMSYA wilaya  katika kuboresha utendaji wa TAMSYA ndani ya halmashauri, ili kufanikisha maendeleo ya wanafunzi na vijana wa kiislamu.

 

Pia Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Ndugu SAID MAJALIWA, aliahidi kushughulikia changamoto mbalimbali za TAMSYA ili kuwawezesha vijana wa Kiislamu kuwa msaada kwa jamii na taifa.

Mgeni rasmi wa mahafali hiyo, Ndugu JUMA MLANDULA, aliwatia moyo wahitimu kuwa waadilifu na kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao yajayo. Pia aliwataka viongozi wa TAMSYA  kuwa na mipango endelevu ya kushughulikia changamoto za TAMSYA ndani ya wilaya ya kilombero ili,Pia alihimiza umma wa kiislamu kuweza kujiandaa na mabadiliko ya sayansi na teknolojia(akili mnemba) ,Mwisho wa hotuba yake, aliahidi kufanyia kazi changamoto zilizowasilishwa kwenye risala rasmi ya mahafali.

 

Kwa kutambua mchango wao, uongozi wa TAMSYA Wilaya ya Kilombero ulitoa zawadi ya kilo 20 za mchele kwa mgeni rasmi na kilo 20 za mchele kwa Mwenyekiti wa Idara ya Elimu TAMSYA Mkoa wa Morogoro kama ishara ya heshima na shukrani kwa ushiriki wao.

Mwisho, Uongozi wa TAMSYA unaendelea na juhudi za kuandaa mahafali kwa lengo la kuwaaga wanafunzi wanaohitimu ili kutambua mchango wao wa kushiriki program mbalimbali za TAMSYA, huku ukiwatakia kila la kheri katika maisha yao ya kitaaluma na kidini.

 

Imetolewa na 
AYOUB JUMA MKONDO.
AMIR-TAMSYA KILOMBERO.