TAMSYA yatembelewa na HESLB

Afisa Habar TAMSYA Taifa.

Katibu Mkuu, Ibn Japhary alipokea Ugeni kutoka bodi ya Mikopo (HESLB), walipo tembelea Katika Ofisi za TAMSYA wakiwakilishwa na Bw. Edward Kilele.

 

Lengo la Kutembelea ofisi lilikuwa ni kuhakiki taarifa za wanafunzi waliofadhiliwa na TAMSYA wakati wa masomo yao, kujenga mahusiano mema na kutoa kutoa elimu kuhusu mikopo na huduma za bodi ya mikopo.

Katika kikao hicho, bodi ilichagiza juu ya kazi za TAMSYA na kusisitiza kuendelea kujitajidi kuwahudumia Kwa Karibu Vijana wa Kitanzania hasa wale walio Katika mazingira magumu ili kuhakikisha wanaweza kufikia malengo yao.

 

Sambamba na kusisitiza kuwa Serikali kupitia Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan -Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameongeza fedha ili kuhakikisha watoto wengi wa Kitanzania wanaweza kumudu gharama za Elimu nchini.

 

Aidha Mwenyekiti Idara ya Elimu Dkt. Semili Pazi aliweza kusisitiza juu ya kuhakikisha wanafunzi wanawezeshwa na bodi kwani elimu ni nyenzo muhimu ya kimeisha hasa katika nyakati hizi za ukuaji WA sayansi na teknolojia.

Katibu Mkuu alipongeza bodi kwa uboreshaji wa huduma na utatuzi wa changamoto za wanafunzi Katika hatua zote za uombaji wa mikopo.

Alhamis,
Oktoba 2, 2025.